Joel 1:18-20

18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!
Makundi ya mifugo yanahangaika
kwa sababu hawana malisho;
hata makundi ya kondoo yanateseka.

19Kwako, Ee Bwana, naita,
kwa kuwa moto umeteketeza
malisho ya mbugani
na miali ya moto imeunguza
miti yote shambani.
20Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku;
vijito vya maji vimekauka,
na moto umeteketeza
malisho yote ya mbugani.
Copyright information for SwhNEN